JINSI YA KUONDOA CHUNUSI

2:45:00 PM

Chunusi husababishwa na kuongezeka kwa uzalishaji wa Testosterone hormone na mafuta yamwili wakati wa mabadiliko ya kimwili pia husababishwa na msongo wa mawazo, matatizo ya kisaikolojia.
Product kama Tea Tree Oil, Aloe Vera, Zinc, and Vitamin A ni vitu vya kihalisi vinavyo weza kutibu chunusi na kuna baadhi ya product hazishauriwi kutumiwa na mtu kama unaujauzito au unatatizo la kiafya hivyo unatakiwa kuwasiliana na dactari kabla ya kutumia kwa ushauri.
Kabla ya kuoga ponda nyanya changanya na asali na maji ya roses na paka nyanya kwenye uso wako kaa nayo kwa muda wa dakika 20 kabla ya kuosha.
Usiku kabla ya kulala paka mchanganyiko wa cream, glycerine, and lemon juice kwenye uso wako na kaa nayo kwa muda wa dakika chake kabla ya kuosha.
Pia jambo la muhumu kwa mtu anayesumbuliwa na chunusi ni kunywa maji kwa angalau lita 3 kila siku pia ni muhimu sana kwa ngozi yako, matunda fresh na mboga za majani kwenye diet yako.
Vitu unavyotakiwa kuepuka ni kugusa uso wako mara kwa mara, epusha nywele kugusa uso wako na kutumbua chunusi kiholela.
Pia epuka kupaka make up nyingi usoni ni vizuri kutopaka make up kabisa ukiwa na tatizo la chunusi.

You Might Also Like

15 comments

 1. asante dia kwa ku2postia hii post na jisi ya kutoa vidoadoa vyeusi usoni vya chunusi au kipelechochote

  ReplyDelete
 2. hapoumenikuna nakushukuru sana sana kwani mie ninatatizo la kutumbua sana chunusi. ubarikiwe kwa kutusaidia.

  ReplyDelete
 3. huduma nzuri kabisa, big up kwa taarifa muhimu.

  ReplyDelete
 4. wa hapo juu umenena jamani mamy 2wekee na tiba ya kuondoa vidoadoa usoni

  ReplyDelete
 5. asante lakini matumizi ya aloe vera hujabainisha

  ReplyDelete
 6. Thanks a lot my dia, nimefurahi ile mbaya kwa tiba ya chunusi jinsi ulivyoielezea nimeelewa na nimependa ile mbaya, ubarikiwe sana. ila bado sijafahamu vitu vya kupaka kama ni cream au lotion kwa ngozi za mafuta my dia tusaidie wadau wako. Tutajie aina ya vipodozi kwa ngozi ya mafuta please.

  ReplyDelete
 7. asante dia.....je naweza vipi kutoa natural spots usoni?

  ReplyDelete
 8. asante nitajaribu njia hizo maana chunusi zinanisumbua ile mbaya na nina uso wa mafuta nakosa hata lotion ya kupaka.asante.

  ReplyDelete
 9. THNX BUT BADO CJAELEWA JINSI YA KUTUMIA ALOVERA KUONDOA CHUNUSI

  ReplyDelete
 10. mbona hujawa wazi cream gani tutumie jamani hili tatizo ni sugu

  ReplyDelete
 11. u lov urslf,do sa directed for beauty you..

  ReplyDelete
 12. JAMANI UMETUOKOA NA SIE TUNAOPIGANA NA CHUNUSI KILA SIKU,UBARIKIWE.ILA MI NAPENDA KUJUA KWA SIE TULIOPO MBALI HYO PRODUCT YA KUUKIMBIA UZEE TUNAIPATAJE?LOV U SISTER NURU

  ReplyDelete
 13. Asante kwa msaada ila pia jaribuni kutumia ukwaju na asali unachanganya pamoja halafu unapaka uson kwa muda wa dk 15 au 20 sio mbaya pia kulala nayo piah kunywa maji kwa wingi inasaidia sana

  ReplyDelete
 14. Asante kwa kutuelimisha kuhusu tatizo la chunusi.je cream gani kwa majina inafaa kwa mtu mwenye chunusi?na sabuni pia kwa jina plz

  ReplyDelete
 15. ASANTE KWA KUTUELEKEZA MY DEAR

  ReplyDelete

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.