Jinsi ya kuondoa mikunjo kwenye ngozi kwa kutumia Aloe Vera Gel

12:21:00 PM

Kabla ya kuanza unatakiwa kujipiga picha ili uweze kuangalia kabla hujaanza kufanya hii treatment na baada ya siku saba ya hii treatment ya kuondoa mikunjo.
Na si kwa ajili ya uso tu ni kwa sehemu zote za mwili.
Nunua chupa ya Aloe vera Gel ambayo unaweza kupata kwenye maduka ya kuuzia madawa ya binadamu au maduka ya urembo.
Safisha uso wako kwa kutumia cleanser yoyote ambayo inaendana na uso wako kama Noxema, Neutorgena, Biore, and Oil of Olay.
Kisha osha na maji ya uvuguvugu always usitumie maji yaliyo na moto sana kusafisha uso alafu ukaushe uso wako.
Weka kiasi cha Aloe Vera Gel kwenye mkono then rub ur hands together (samahani kiswahili kigumu) alafu paka kwenye uso wako avoid isiingie kwenye macho.
Baaada ya kupaka Aloe Vera Gel unaweza kupaka cream unayotumia au lotion kwenye uso ila usisubiri Aloe Vera Gel ikauke .

You Might Also Like

11 comments

 1. Mm niko nje kidogo na mada utanisamehe mpzn shida yangu kubwa mm ni uso wangu yaani una matatizo sana, ngozi yangu ya mwili ni kavu usoni ni full mafuta ma dia yaani nina chunusi nyingi makovu mengi sana yaani hata sitamani kujianglia kwenye kioo nimehangaika na kutumia hela nyingi lakini wapi, naomba unishauri manake sasa nimechoka jamani naombeni msaada wenue wa dau niondokane na tatizo hili. Nilipokuwa secondary niliumwa na ungonjwa wa ngozi ninavyokwambia hadi sasa ninamadoa kwa kweli yananiboa sana, mm natamani niwe mrembo kama wadada wenzangu nahitaji msaada.

  ReplyDelete
 2. Tunashukuru mamaa kwa kutuelimisha juu ya hii treatment lakini ningependa kujua Je! unatakiwa kufanya mara ngapi kwa siku?

  ReplyDelete
 3. Asante mpendwa kwa kutufanya tuonekane vijana, mimi nina tatizo moja, naomba nielekezwe jinsi ya kuondoa mistari inayotokea kwenye mikono, tumbo mapajani hasa kwa watu wanene, wengine inawatokea baada ya kupaka cream, lakini mimi ni kwaajili ya unene.

  ReplyDelete
 4. Hi! sorry hii tretment yako haimfanya mtu akabadilika sura mweusi akawa mweupe?
  goodday

  ReplyDelete
 5. sorry, sura je haikomai kweli?..

  ReplyDelete
 6. naomba ushauri wa cream gani nipake usoni;mie ni mweusi uso wangu wa mafuta.hongera kwa kutuelimisha.

  ReplyDelete
 7. Hi!
  Mimi ngozi yangu ni kavu kuanzia mwili hadi uso, sasa naomba ushauri nipake cream gani ambayo itanifanya niwe mrembo

  ReplyDelete
 8. hey
  nasoma kweli juu ya urembo, but tatizo uso wangu una mafuta mengi tu sana.ushauri wako naufwata but majibu sijayaona mazuri pliz nisaidie ama mi ndio najichanganya......

  ReplyDelete
 9. Asante kwa ushauri dada, kwa kweli nimenufaika sana binafsi na posts zako mbalimbali. Tatizo linalonikabili ni ngozi yangu ina mafuta japo haina chunusi sana ila haiko laini kama ya wengine . mara nyingi nikitumia product yoyote natoka kama vipele vidogo vidogo . Rangi yangu ni nyeusi . ninaomba ushauri hasa kwa kitu ambacho naweza kutumia nikawa soft kama wengine bila kujichubua rangi yangu ni mweusi,

  ReplyDelete
 10. asante kwa ushauri je hiyo aloe vera gel inapatikana wapi?

  ReplyDelete
 11. Asante kwa ushauri naomba kuongezea kuna Sabuni inaitwa Mena Soap ni nzuri mno kwa chunusi na ngozi yenye mafuta

  ReplyDelete

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.