Make up kwa ngozi yenye mafuta

12:11:00 PM

Kama wadau walivyoomba kuongelea mada hii ya make-up kwa ajili ya ngozi zenye mafuta unachotakiwa kufanya kama ngozi yako ina mafuta chagua cosmetics na facial ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya ngozi ya mafuta (ZIMEANDIKWA KWENYE KILA MAKE UP)


Tumia cleanser kusafishia uso wako na unapokua unasafisha uso usisafishe kwa nguvu maana itasababisha ngozi kubaki kuwa ngumu.
Massage uso wako ukiwa unasafisha kisha osha kwa maji ya moto ili kuondoa mafuta.
Unaweza tumia mad or clay mask mara mbili kwa week.
Unaponunua product hakikisha unaangalia lebo kama imeandikwa ni kwa ajili ya ngozi za mafuta au la kwa sababu kuna baadhi ya product unatakiwakuziepuka na na nyingine unatakiwa kuzitumia kama make-up kwa ngozi ya mafuta.
Jiepushe na product zenye alcohol kwa sababu husababisha ngozi kukauka na product zenye petrolium zina mafuta sana na husababisha kufunga kwa vitundu vya hewa kwenye  ngozi.
Tumia free oil make-up au make-up ambazo ni maalumu kwa ajili ya ngozi ya mafuta.
Moisture utakayo tumia hakikisha inakua ni oil-free na sehemu ambazo zinaweza kuhitaji sana moisture ni sehemu ya kuzunguka macho.
Pia unaweza kupaka maji ya matango kwenye uso wako kabla ya kupaka make-up inasaidia sana kwenye muonekano wa ngozi.
Tafuta foundation ambayo ina `titanium dioxide` ambayo pia inasaidia kukukinga na jua.

kila la kheri

You Might Also Like

2 comments

  1. kama mimi nina ngozi ya mafuta nitumie asali na parachichi au na asali tu plz naombeni mnishauli.plz check me stercyllicious@yahoo.com nimejaribu kujiunga na blog hii nimeshidwa

    ReplyDelete

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.