,

JINSI YA KUWEZA KUITAMBUA NGOZI YAKO NI YA AINA GANI

12:51:00 PM

 
Ni vizuri sana kwako kuweza kujua aina ya ngozi yako maana itasidia wewe uweze kuitunza ngozi yako vizuri.Vile vile itakusaidi katika kujua ni vipozi vya aina gani utumie kutokana na ngozi yako. Hakuna ngozi mbili ambazo zinafanana exactly ila zinatofautiana ambapo inawezekana ngozi yako ikawa ni Ngozi Kavu, Ngozi ya Kawaida, Ngozi ya mafuta na ngozi mchanganyiko yaani combine skin. 
 
Ili kujua ngozi yako ni ya aina gani osha uso wako kwa kutumia sabuni ya kusafishia uso then baada ya dakika 30 chukua tishu na futa sehemu ya paji lako la uso, kwenye pua, kidevu na mashavu. 
 
Kama tishu hiyo haitaonyesha kuwana mafuta baada ya kufuta basi ngozi yako itakua ni aina ya ngozi kavu. 
 
Ngozi kavu huwa inaonekana rough na hukabiliwana mistari na wrinkles lakini kama ngozi yako kuna sehemu nyingine inakua kavu sehemu nyingine inakua na mafuta basi ngozi yako itakua ni ngozi mchanganyiko. 
Ngozi ya kawaida au Normal skin huwa inaonekana laini na ngozi hii ya mafuta ukiigusa unayahisi mafuta na huwa inang`aa. Ngozi hii ya mafuta huwa inakabiliwa sana na blackheads na pimples/chunusi na kwa kuwa ngozi hii ni sensitive inahitaji special care na umakini na vipodozi unavyopaka kwenye uso wako. 
 
Kwa watu wenye ngozi sensitive kama hii ni lazima kutumia misaada ya ushauri kwa wataalamu wa ngozi ili kulinda ngozi zao kupata mzio/allergic. Ni lazima mara kwa mara uwe na utaratibu maalum wa kuihudumia ngozi yako kulingana na mahitaji ya ngozi yako na huenda ikachukua muda mrefu kwa ngozi yako kurudia hali ya kawaida kuweza kuondokana na hili tatizo.

You Might Also Like

5 comments

 1. Habari za mishughuliko, kwa kweli nimeipenda sana hii mada ya kujua ngozi yako, nami ni muathirika wa ngozi mimi ngozi yangu ina mafuta sana hivyo nilikuwa naungua sana kuzunguka macho kila nipakapo cream yeyote ikatokea nikakutana na watu wanaouza bidhaa za GNLD wakanishauri nipakae product zao kwa kweli nilijitahidi nikanunua ingawa ni gharama kubwa lakini matokeo yake nikawa na weusi unaozunguka uso nimehangaika sana jamani hadi sasa nakata tamaa, ngozi inakuwa ina kama layer nyingine ya juu, naomba kama unaweza nishauri nifanye nini au hata kana kuna mdau ambaye anaweza kunisaidia nitashukuru sana. Asante

  ReplyDelete
  Replies
  1. Habari. Tatizo hilo inapendeza likitibiwa kwa njia asili. Japo huchukua mda mrefu ila matokeo mazuri ni uhakika. Mm pia ni muhanga wa tatizo kama ilo. Imechukua mwaka 1 kujitibu kwa njia asili. Ki ufipi. 1. Kunywa maji mengi 2. Lala mda mwingi 8hrs na hakikisha uso wako haugusi sehem chafu. 3 mazoezi pia ni muhim. 4 matunda hasa ya vitamin e. 5.usitumie cream yyte mda huo wala sabuni ya cream.

   Delete
 2. Jamani mimi Nina ngozi y'a mafuta Nina chunusi ajabu yaani nakosa raha na huu uso Nina black spot uso mzima, naomba msaada wako kama ni dactari nikamuone na nitampata hivi? Au kama ni vipodozi unishauri nakuomba sana,

  ReplyDelete
  Replies
  1. My dear, nakushauri tafuta antibiotics za acne( google search acne antibiotic,mimi nilikua na sura kila mtu anaeniona ananiuliza napaka nini wakati niko Tanzania, nimehama nchi tu miezi 9 baadae sura ilikua haifai, nimetumia products za gharama ndani ya miaka 4.. Lakini nilipojifungua( kwa operation) nikapewa dose ya antibiotics, iliondoa chunusi zote usoni. Nikaenda kumuona dr wangu nikamwambia kilichotokea- akanipa oxytetracycline( dose ya miezi 2). Sasaivi sura yangu Kama ya mtoto... Pass on the word. Mungu atakubariki ukisaidia na wengine. Stay blessed and chunusi zitaisha( that's if ni infection Kama niliyokua nayo).all the best

   Delete
 3. Jamani tunahitaji msaada wa namba za simu za wataalam wa ngozi maaana tunasumbuliwa sana na hawa wanaojiita walaam wa ngozi kumbe ni watengeneza mikorogo feki ngozi yangu ni ya mafuta nahitaji msaada wa haraka na wenye kufaa

  ReplyDelete

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.