MASK YA ASALI, YAI, MAFUTA YA ALMOND/MLOZI NA MAZIWA YA MTINDI KWA NGOZI KAVU

7:27:00 AM

 
Bado huu ni mwenyelezo wa jinsi ya kutumia mask kwa ngozi za aina tofauti na bado niko kweney ngozi kavu lakini hapa tunaangalia mchanganyiko mwingine wa kutumia asali, yai, mafuta ya mlozi/almond oil na maziwa ya mtindi.
Kinachohitaji :

  • Kijiko 1 cha asali
  • Yai 1 kiini chake
  • 1/2 kijiko cha mafuta ya almond/mlozi
  • 1 kijiko maziwa ya mtindi
Kama kawaida changanya mchanganyiko huu kwa kutumia bakuli kubwa na koroga mpaka inakuwa inanata na isiwe nzito sana. Paka mask kwenye uso wako kuyazunguka macho na midomo yako na kaa nayo kwa dakika 20 kisha nawa kwa sabuni unayotumia kusafishia uso na maji ya uvuguvugu na rudia tena kwa maji baridi. 

Asali inasaidia kuufanya usoo wako uwe smooth wakati yai na mafuta mlozi/almond oil kupenya na kumoisturize uso wako , na maziwa mtindi yanasidia kusafisha matundu kwenye ngozi na kuyafanya yawe tight..Pia mchanganyiko huu unasaidia kuondoa mikunjo katika ngozi na fanya mask hii mara moja tu kwa wiki..

Endelea kutembelea nitaendelea kuwafahamisha zaidi ni mask gani utumie kwa aina ya ngozi yako.

You Might Also Like

1 comments

  1. HIYA ALMOND OIL NITAIPATA WAPI MY DEAR.

    ReplyDelete

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.