MASK YA USO KWA NGOZI ZA AINA TOFAUTI

3:28:00 PM

Kuna njia rahisi za kutengeneza mask ya uso kulingana na ngozi za aina tofauti kwa kutumia asali. Kuna hatua na vitu vinavyohitajika kutengeneza mask ya asali ambapo inatumia muda kidogo. Kwanza unatakiwa kuchagua mask hii ya asali kulingana na ngozi yako.

Kwa ngozi kavu: Mask ya uso ya Parachichi/Ovocado na Asali

Unahitaji:
  • Vijiko 2 vya chakula vya avocado
  • Vijiko 2 vya asali
  • Yai 1 lakini ni kiini/yolk

Ili kuchanganya ingredients hizi pamoja vichanganye vyote kwenye blenda au viponde kwa mikono katika bakuli ili vichanganyike.

Kisha tumia vidole kueneza mask juu ya uso wako mpaka kwenye shingo na iache kwa muda wa dakika 30 kabla ya kuondoa na kisha safisha uso wako kwa maji ya uvuguvugu. Kwa wenye ngozi kavu unatakiwa kufanya mask hii mara moja kwa wiki.Endelea kutembelea blog nitaendelea kukueleza vitu vya kutumia kwa ngozi nyingine tofauti na ngozi hii kavu.

You Might Also Like

1 comments

  1. kama mimi ngozi yangu ni ya mafuta nipake kwa mda gani??see me on stercyllicious@yahoo.com please help!!

    ReplyDelete

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.