KUTOKA KWA MDAU: JINSI YA KUONDOA MAKOVU,CHUNUSI NA BLACKHEAD

12:25:00 PM

kuhusu makovu, jaribu kutumia bio oil, matokeo yake ni polepole ila ya uhakika na hamna kemikali.. Na pia makovu ya mfano kwenye magoti, (weusi wa magoti) unaweza ondoa kwa kupakaa juisi ya limao, acha dakika 10-15. Kisha chukua pamba, ichovye kwenye maji ya uvuguvugu na sugua magoti, weusi utaanza kupungua..

Na wale wote wenye chunusi usoni, na blackheads, jaribu kuosha usho wako (tumia cleanser ambazo hazi -irritate ngozi yako, ambazo hazina kemikali) kila siku asubuhi na jioni kabla ya kulala. fanya mask ya kuchanganya asali na limao (waweza fanya kila siku), asali na mdalasini (mara 2 kwa wiki), dakika 15-20 osha na maji ya uvuguvugu. pakaa lotion yako.

Waweza kuondoa blackheads kwa kutumia ute mweupe wa yai, toa kiini cha yai, pakaa ute usoni, tafuta vitambaa laini cheupe hata vitatu, ukishapakaa ute, bandika kitambaa juu yake, acha dk 20, halafu bandua kitambaa, utaona vinatoka na blackheads.

Sheria zingine kwa wenye chunusi,
- Acha kushika uso wako na mikono, jitahidi mikono isiende usoni kila wakati, mara nyingi inakuwa na bacterias
- Osha mikono yako kabla hujaanza kupakaa/ kuosha uso wako
- Tumia vipodozi ambavyo havina kemikali nyingi, vipodozi vya watoto ni vizuri zaidi
- Kunywa maji mengi hata lita 2 kwa siku
- Acha stress
- Acha kutembea na kioo, n akujiangalia usoni kila dakika
- Acha kutumbua chunusi, zinakuletea mabaka meusi..

Jaribu nilivyokushauri hapo juu, japo hata kwa wiki 2 na utaona matokeo yake, mi pia nilikuwa na chunusi, kwa kufuata hizo taratibu, lol naweza kwenda nje bila makeups.

Zingatia Usafi!.. mdau kutoka Uholanzi!

You Might Also Like

1 comments

  1. Jee kwa wenye makovu ya kuumia inakuaje????!!!kuna dawa ya kuyaondoa?mana yangu yananikera mno.....!

    ReplyDelete

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.