,

FAHAMU JINSI YA KUTUMIA YAI & YOGURT KUTENGENEZA HAIR MASK KWA AJILI YA NYWELE ZAKO.

8:00:00 AM

Hair mask ni rahisi kutengeneza na it is cheap kuliko conditioner, ila unaweza pia ukatumia conditioner baada ya kutumia hair mask, ukitumia hizi hair mask unakua kama unazilisha nywele zako. Mfano mayai na yogurt inazipa nywele zako protein na kuzifanya ziwe laini, nzito na ziwe zina'ngaa. Hii hair mask ni znuri kwa wote ila sana sana kwa wale wenye nywele zilizo haribika na kavu.


Jinsi ya kutengeneza::
Chukua mayai 2, yogurt, ndimu na olive oil.

Chukua mayai, kwa wale wenye nywele zenye mafuta sana tumia lile yai la nje tu, kwa wale wenye nwele kavu tumia kiini cha yai tu, na kwa wale ambao nywele zao ni za kawaida tumia yai zima.Weka kwenye bakuli na  likoroge vizuri.
Weka kikombe kimoja cha yogurt pamoja na vijiko 2 vikubwa vya olive oil kwenye bakuli then changanya vizuri, then kamulia ndimu moja na uendelee kuchanganya.

Paka mchanganyiko wako kuanzia kwenye ngozi ya kichwa hadi kwenye nywele zako huku ukiwa kama una massage, hakikisha nywele zote zimeshika vizuri.

Vaa disposable shower cap ili isichuruzike kila mahali na ukae dakika 15.

Osha na maji ya kawaida au ya baridi. Usitumie maji ya moto, kumbuka kwamba umetumia mayai ukiosha na maji ya moto mayai yatabaki kwenye nywele.

Then tumia shampoo uipendayo kuosha nywele zako, tumia yenye harufu nzuri ili kuondoa harufu ya mayai.You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.