JIFUNZE JINSI YA KUCONTOUR USO WAKO MWENYEWE PART 1

7:00:00 AM


  • Contouring inafanya uso wako uonekane more defined, na ili uweze kupatia vizuri unatakiwa kujua uso wako ni shape ipi, maana kila mtu sura yake ni tofauti na hivyo unatakiwa uiwezee sura yako. Angalia hii picha inaonesha aina za shape ya sura
  • Kama inavyoonesha hapo kuna oval, long, round, square, heart na diamond na zote zina njia yako ya ku contour.

  • Vitu utakavyohitaji::
  • Angled Brush
  • Blusher Brush and blush
  • Bronzing Brush and bronze
  • Highlighter (powder/creme)
  • Flat Brush
  • INGIA HUMU KUONA AINA ZA MAKEUP BRUSH

Anza kupaka makeup yako kama kawaida, pale ukisha paka foundation ndio inafuata contour, hakikisha foundation yako ishatulia usoni.
Ukiwa tayari, fanya kama unavuta mashavu yako kwa ndani utaona kama imejitengeneza alama ya B. Then tumia angled brush blusher brush kupitisha bronzer kwenye hiyo B inayotokea katika cheekbones zako. Fanya kama una sweep kutoka kwenye sikio pale moja kwa moja hadi karibu na mdomo (juu ya jawline yako)

Ukisha blend vizuri bronzer yako, chukua blush na brush yake pitisha kwenye cheek bones na jaw line, na ka wale wenye videvu viwili pitisha bronzer chini ya kidevu kukifanya kionekane kidogo.

Then chukua bronzing powder yako na upitishe pembeni mwa pua upande zote mbili na kati pitisha highlighter.

Pia kuna pua tofauti..na jinsi ya kuzi contour

Kwa highlighter kama unatumia creme highlighter hakikisha isigusane na na powder. Angalia sehemu ambazo jua linapiga ndio upake. Kama unatumia ya creme paka kwa kutumia vidole, kama ya powder tumia brush lake.

Anza katikati kwenye pua, kwenye mbinuko wa nyusi zako, kwenye paji la uso na kwenye mashavu (cheekbones.)
Wengine wanapaka kwenye corner ya macho na kwenye ile M ya kwenye lips za juu.

Then malizia na blush

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.