MATUMIZI 7 YA MATANGO KUPATA NGOZI YENYE AFYA/CUCUMBER FOR HEALTHY SKIN.

12:20:00 PM

Matango sio ya kula tu..yanaweza kutumika kufanya ngozi yako iwe nzuri na yenye afya..shuka chini kujua matumizi yake zaidi::

1.Inaondoa weusi chini ya macho/Fades away dark circles
Matango yana antioxidants & silica ambayo husaidia katika kuondoa weusi chini ya macho. Cha kufanya ni kuchukua vipande viwili vya matango ma kuweka macho huku umerelax kwa mda wa kama dakika 20.

2.Inapunguza kuvimba kwa macho/Reduces puffy eyes
Matango pia yana ascorbic acid ambayo husaidia kupunguza uvimbe wa macho..napo unaweza kukaa na matango kwa dakika 20 au kutumia pamba kupaka majimaji ya matango maeneo ya kuzunguka macho.

3.Huondoa vipele na madoa usoni/Fades freckles.
Matango pia unaweza kutumia kama tonic..saga au kwangua tango..ila ni bora kulikwangua kama vile unavyokwangua carrot..then paka usoni hadi shingoni.

4.Inafanya uso wako kuwa fresh na laini/Improves complexion
Hapa ukitumia matango kama facial mask..ile juice ya matango changanya na juice ya ndimu na kupaka usoni..inafanya uso wako u glow, kuondoa makovu na pigmentation.

5.Husaidia kurejuvinate ngozi baada ya kuungua kwa jua/Treat a sunburn.
Yes, hata watu weusi wanaungua na jua lakini sio sana kama wazungu..so matango pia yatakusaidia kurudisha ngozi yako katika hali ya kawida baada ya kuungua na jua.

6.Inaziba vishimo usoni/Tightens open pores.
Unaweza pia kutumia matango ku tighten your pores usoni, tumia kama toner kwa kuchanganya na apple cider vinegar, ndimu kidogo, asali, aloe vera gel na nyanya au unaweza kutumia yenyewe tu.

7.Inaondoa cellulite.
Chukua nusu kikombe ya ground coffee, asali ya kutosha na juice ya matango ya kutosha. Changanya vizuri kisha paka mchanganyiko kwenye sehemu yenye cellulite, funika kwa kutumia muslin wrap sheet na baada ya dakika 30 fanya kama una scrub polepole. Unaweza pia ukala matango kila siku ili kuweza kuepukana na cellulite.


You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.