, , ,

FACIAL FRIDAY :: KWA NGOZI YENYE MAFUTA, INAONDOA CHUNUSI/BLACK HEADS/WHITE HEADS

12:49:00 PM
Hii facial ni nzuri kwa wanawake wenye matatizo na ngozi,kama una chunusi basi hii inaondoa, inatoa pia ngozi iliyokufa, inakinganisha rangi ya ngozi yako, sio sehemu moja mweupe sana alafu sehemu nyingine mweusi..na pia kuifanya ngozi yako laini.

Vitu unavyohitaji ::


  • Yai 1
  • Toilet paper au Napkin.


Tenganisha yai la nje na kiini, weka kwenye mabakuli tofauti..na uyakoroge yote kivyake.


Nawa uso wako vizuri, then paka yai la nje usoni kote kasoro sehemu inayozunguka macho na mdomo.

Chukua napkin/toilet paper na uweke juu ya uso, hakikisha umeacha vitobo vya macho na mdomo. Kama yai lako la nje bado limebaki, basi chukua na upake tena kwa juu ya hiyo napkin/toilet paper. (ukizidisha itachukua mda mrefu kukauka)

Subiri dakika 20-30 hadi itakapokauka, hiyo napkin/toilet paper itakuwa kavu kabisa the toa haraka kwenye uso.

Nawa uso, then paka kiini cha yai ili ngozi yako iwe hydrated na kulainika. Subiri dakika 10 then nawa uso. Utagundua kuwa uso umekua laini na msafi.

Hii mask sio kwa ajili ya ngozi aina zote, inafaa kwa wale wenye ngozi zenye mafuta kwasababu inatoa mafuta usoni na kuepusha chunusi kutokea. Inafaa pia kwa wale wenye hyper-pigmentation.(Bonyeza HAPA kusoma kuhusu pigmentation usoni).
Hifai kwa wale wenye ngozi sensitive!


You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.