, , ,

FACIAL FRIDAY :: PARACHICHI, NDIZI & OLIVE OIL

3:42:00 PM

Facial Friday means another facial mask unayoweza kutengeneza mwenyewe nyumbani na kupata ngozi nzuri kwa kutumia vitu asilia na sio vyenye machemical makali.

Hii facial mask ni rahisi tu kutengeneza  na vitu ambavyo tunaviona kila siku, unatumia ndizi, parachichi na olive oil. Olive oil unaweza kupata katika maduka ya urembo au hata super market. Chukua olive oil ya mwili na sio yale ya kupikia. Maparachichi yana antioxidants zinazosaidia ngozi isijikunje na pia ni moisturizer asilia..kitu natural.

So all you need kutengeneza hii facial nyumbani kwako ukiwa umerelax ni Ndizi nusu iliyoiva, Parachichi nusu na kijiko kimoja tu cha olive oil.

Toa maganda ya ndizi na parachichi, then weka katika bakuli, ongeza kijiko 1 kikubwa cha olive oil kisha ponda ponda vizuri hadi ichanganyike..unaweza pia ukaweza katika blender ichanganyike vizuri.

Kama unafanya full spa day nyumbani kwako mwenyewe basi ni vyema kupaka hii facial mask baada ya kufanyia scrub uso wako.
Ukishaufanyia uso wako scrub, utakuwa umenawa uso wako, kausha vizuri kwa taulo then paka mchanganyiko wako usoni, hakikisha unaepuka sehemu inayozunguka macho. Kaa nayo kwa muda wa dakika 15.

Nawa kwa maji ya uvuguvugu then kausha uso pole pole kwa taulo safi.

 Paka moisturizer and spend the rest of the day bila makeup..acha uso upumue hata kwa siku 1.

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.