, , , , ,

JINSI YA KUCHORA/KUJAZA NYUSI ZAKO KWA KUTUMIA BROW POWDER.

7:00:00 AM

Kabla sijaanza kujihusisha na mambo ya makeup ni vitu vingi sana nilikuwa sivijui na nadhani kuwa bado wapo wale wasiojua utaratibu wa makeup vizuri, kama vile makeup products au makeup tools..na hivyo kuna wengine bado wanatumia wanya wa kawaida kujazia/kuchorea nyusi zao, hiyo pia ni sawa lakini brow powder ndio better zaidi.

Kuna brow powder aina nyingi, zingine zinakuwa zimeandikwa kabisa brow kit/brow powder /eyebrow powder kwa juu au kwa chini. Ni vizuri ukachukua rangi ya brown na nyeusi au uliza mtu anayeuza akiweza kukurecommend kutokana na rangi yako.
Jinsi ya kujaziliza/kuchora nyusi zako.
Uwe na brow powder. eyebrow brush (ingia humu kujua aina za brush) na concealer.
Anza kwa kuzichana nyusi zako kwa kutumia spoolie brush, kama hauna tumia kitana kidogo, then chukua brow brush yako na uchukulie brow powder kisha uanze kupaka.
Kama haupo vizuri katika kupaka unaweza kutumia eyebrow shaper (angalia hapa video ya da zeze akitumua eyebrow shaper) na uchore shape inayokufaa.
Then chukua foundation yako ili usawazishe ile iliyotokeza/kunyoosha ule brow powder. Tumia concealer brush kupaka mstari mwembamba ulionyooka ukifuatisha uliyochora au kujaziliza nyusi zako. Fanya hivi kwa juu na chini kisha sawazisha vizuri.


Angalia this video by Alexis Kaymor Uweze kuelewa vizuri.

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.