, , , ,

JINSI YA KUONDOA VIPELE/CHUNUSI KICHWANI (SCALP ACNE)

3:47:00 PM

Kwa wengine vipele/chunusi huwatokea kichwani kama inavyotokea usoni. By kichwani namaanisha ngozi ambapo nywele huota, na vinakua vinauma. Usipojitahidi kuvitibu unaweza ukapata matatizo mengine. Ukiwa unajikuna sana sehemu hiyo inazidi kulika na kusababisha nywele kuanza kukatika. 

Njia zifuatazo zitakusaidia kuondoa vipele/ chunusi kichwani::
Tumia Tea Tree oil, changanya na olive oil au coconut oil kisha massage kwenye ngozi yako kichwani. Unaweza pia ukachangaya katika shampoo yako na kuoshea nywele zako.
*watu wengine wanaweza kuwa allergic na tea tree oil hivyo jaribu kwanza kufanya patch test mkononi kaa nayo kwa dakika chache ili uje kama upo allergic nayo au la*

Tumia binzari manjano/tumeric kijiko nusu changanya na mafuta ya nazi/coconut oil upate mchanganyiko mzito, paka katika sehemu zilizo kuwa affected..kwa kwa lisaa 1 kisha osha kwa shampoo. Fanya hivi kila siku au mara 2 kwa wiki kwa wenye busy schedule.

Tumia apple cider vinegar kipimo sawa na maji ya uvuguvugu, changanya. Baada ya kuosha nywele zako fanya kama unalowanisha tena nywele zako na huo mchanganyiko, baada ya dakika 7, kisha suuza tena nywele zako na maji masafi. Usipake hiyo apple cider vinegar peke yake, nilazima uchanganye na maji.
Fanya hivi kila ukiosha nywele zako.

Tumia Aloe vera.. unaweza ukachukua jani na aloe vera likate na uchukue ile pure gel yake na kupaka sehemu zilizoathirika mara 2 kwa siku kwa wiki 2.

Au  chukua nusu kikombe cha Aloe vera gel na ndimu nusu kisha changanya, paka kwenye nywele zilizolowa huku uki massage polepole. Kaa nayo kwa dakika 10 then osha nywele kwa maji ya uvuguvugu.

Tumia tomato juice/juice ya nyanya...paka juice ya nyanya kisha osha nywele kwa maji ya uvuguvugu baada ya dakika 10.

 Au chukua juice ya nyanya na uchanganye na ndimu nusu na asali kisha paka sehemu zilizokuwa affected..kaa dakika 5 kisha osha.

Tumia kitunguu swaumu/garlic...vina antioxidants zinazosaidia kuponya vipele na hata vidonda kichwani, na kupunguza maumivu. Chukua vitungu 4 au 6 na vikombe 3 vya maji kisha bandika maji yachemke, ipua toa vitunguu swaumu , funika na uache maji yapoe. Yakishapoa, osha nywele zako kwa maji haya kisha subirikwa dakika 10 na uoshe kwa maji masafi. Fanya hivi mara 1 kwa siku.

Tips za kuepusha scalp acne/ vipele au chunusi kichwani.
  • Osha nywele zako mara kwa mara, angalau mara 1 au 2 kwa wiki kuepusha uchafu usijikusanye kichwani na kuziba pores.
  • Hakikisha vitana, chanuo, vibanio na hata mataulo yako ni masafi kabla hujatumia katika nywele zako.
  • Ukiwa unaosha nywele zako, fanya kumassage kichwa chako polepole ili uchafu utoke.
  • Kama tayari una tatizo hili kaa mbali na greasy products kama  gel na hairspray.
  • Acha kutumia conditioner kwa muda hadi upone, au paka tu kwenye nywele za juu.
  • Usinyoe nywele kipindi una scalp acne
  • Usijikune, badala yake chukua taulo weka kwenye maji ya moto (sio sana) na uwe kama unakanda sehemu inayowasha.
  • Kunywa maji ya kutosha.

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.