, , ,

5 EXERCISES ZA KUONDOA MANYAMA UZEMBE/LOVE HANDLES.

4:00:00 PM


Kwa sisi wanawake ni rahisi sana kupata manyama uzembe, yanani zile nyama za pembeni mwa tumbo ndio wanaita Love handles. Hivyo kama na wewe wataka kupunguza manyama uzembe basi fanya haya mazoezi 5 huku ukiwa upo katika healthy diet na ukiendelea kufanya full body workout/mazoezi ya mwili mzima..lakini kama unataka kuondoa manyama uzembe tu basi fanya haya mazoezi huku ukiwa unakula healthy.

1.Simama vizuri huku umeshikila weight ndogo tu, kama unafanyia nyumbani na huna weights basi chukua chupa kubwa ya maji litre 1.5 na ujaze mchanga. Ishikile weight/chupa uliyotengeneza juu ya kichwa kisha pindisha mkono upande wa kushoto kidogo huku ukinyanyua mguu upande huohuo wa kushoto, rudisha chini kisha rudia reps 15. Fanya hivyo vivyo kwa upande wa kulia.

2.Kaa mkao wa kupiga push-up (plank position), hakikisha kichwa na mgongo umenyooka na miguu imeshikana. Hop mbele upande wa kushoto then rudi position ile ya mwanzo, rudia hivyo hivyo kwa upande wa kulia. Fanya reps 20 kwa kila upande.

3.Side plank deeps, lala kushoto kiupande, the jinyanyue kwa mkono mmoja na mkono mwingine shika kiuno chako. Hakikisha mguu wako upo juu ya mguu wa kushoto, na uwe umenyooka. Then shusha hips chini lakini usifike hadi kwenye floor, then rudi juu position uliyokuwa umekaa mwanzo. Rudia reps 20, then fanya hivyo hivyo kwa upande wa kulia.

4.Squat jump, chukua tena weight /chupa yako yenye mchanga, shikilia kama hapo chini then squat, badala ya kuinuka tu kawaida kama squat unayofanyaga, ruka juu na ugeuke utue upande mwingine position ileile ya kusquat. Reps 15 kila upande.

5.Spider man, kaa position ya kufanya plank, nyanyua mguu wa kushoto huku umeukunja, uvute kwenda mbele hadi goti lishikane na mkono wa kushoto, then rudisha ulipokuwa. Fanya hivyo hivyo kwa upande wa kulia.

Then ukiwa umeshafanya hivyo pande zote mbili na umerudi in a plank position, chukua tena mguu wa kushoto uvute juu lakini this time ukashikane na mkono wa kulia..fanya hivyo na mguu wa kulia ushikane na mkono wa kushoto.

Unaweza ukarudia tena round nyingine ukimaliza hapa, na kama mguu wako haufiki kushikana na mkono usijali, siku zinavyozidi kuenda utaona progress polepole.
Kumbuka ukiwa unafanya haya mazoezi uwe unakula healthy.

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.