, ,

SEA SALT INAWEZA KUKUSAIDIA KUONDOA CHUNUSI SUGU/ACNE

12:14:00 PM


Kuna wale wanaosumbuliwa sana na chunusi, na kila kitu anachojaribu kutumia kuondoa hizo chunusi haifanyi kazi. YouTube beauty vlogger April Bee alikuwa anasumbuliwa naye kwa miaka kadhaa na hatimaye akaweza kupata njia iliyomsaidia kuondoa hizo chunusi/acne.

Sea salt inaua bacteria, ina-restore PH balance, ina minerals,vitamins na ina exfoliate na kulainisha ngozi.
Alitumia njia asili kabisa, na vitu kama sea salt/chumvi ya baharini kutengeneza toner pamoja na facial mask.
 Sea salt toner for Acne(chunusi)

  • Kikombe 1/4 cha distilled water.
  • Kijiko 1 cha sea salt.

*Distilled water ni maji yaliyotolewa impurities zote. Ingia HAPA kujua jinsi ya kutengeneza. Au unaweza kununua.

Weka hayo maji na chumvi katika saucepan na ubandike jikoni kwenye moto mdogo sana. Koroga hadi chumvi iyayuke then ipua na uache ipoe. Weka kwenye spray bottle, kama huna tunza kwenye container imara. Kutumia, nawa uso wako vizuri, chukua mchanganyiko wako na uspray/paka kwa kutumia pamba kwenye uso msafi. Acha ikauke then nawa kwa maji ya uvuguvugu kisha paka moisturizer.

Sea salt mask.

  • kikombe 1/4 cha aloe vera gel.
  • Kijiko 1 na nusu cha sea salt.


Changanya katika bakuli, then tumia brush laini kupaka usoni(makeup brush), kaa nayo kwa dakika 30, then nawa kwa maji ya uvuguvugu then moisturize.

*Hakikisha sea salt utakayotumia hai-contain Iodide na ingredients zilizopo ni sea salt tu.
Angalia this short video ya April Bee akituonesha jinsi ya kutengeneza sea salt toner na mask.You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.