, , , ,

JINSI YA KUFANYA FACIAL NYUMBANI / HOW TO DO A FACIAL AT HOME.

8:00:00 AM


Ladies leo nimewaletea a step by step process itakayokuwezesha kufanya facial mwenyewe nyumbani. And kama kuna topic yoyote mnayohitaji kuletewa feel free kuaca comment hapo chini au tufollow kwa our Instagram page :: BONGOUZURI, acha comment au tuma DM (Direct Message) na utaletewa topic au kujibiwa maswali yako.
*Toa makeup yote kabla hujaanza.
STEPS.
1.CLEANSE THE SKIN / SAFISHA USO WAKO.
Inapokuja kwenye kusafisha uso wako, wengi wananawa uso na sabuni tu kama kawaida, lakini kuna wengine wanatumia a specific cleanser ambayo inafaa kwa ngozi zao ndio maana unamkuta mtu ana ngozi laini na safi bila madoa.

Hivyo ni vizuri kama ukiweza tafuta cleanser ambayo itafaa ngozi yako, kuna cleanser za wenye ngozi ya mafuta, wenye ngozi kavu, na wenye ngozi ya kawaida (ingia HAPA au HAPA kujua aina ya ngozi yako)..na pia zina ingredients tofauti, hivyo ni vizuri kama utafanya uchunguzi kabla haujaenda kununua tu cleanser yoyote.

Nawa uso na shingo kwa maji ya uvuguvugu kwanza, USITUMIE YA MOTO!. Then chukua cleanser yako paka kwenye paji la uso, mashavu na kidevu kisha anza ku-massage na kusambaza uso mzima hadi kwenye shingo angalau kwa dakika 1.

Chukua wash cloth/kitambaa laini na maji ya uvuguvugu utumie kusafishi uso hadi cleanser yote itoke.

2.EXFOLIATE YOUR SKIN.
Hapa ndipo pa kutumia scrub..baada ya ku-cleanse chukua scrub yako unayotumia, kama huna unaweza kupata katika maduka ya urembo au ukatengeneza mwenyewe, katika post za nyuma utakuta facial scrubs kama HII .

Paka scrub yako usoni, kisha zungusha katika mduara pole pole, uso mzima. Sanasana concentrate katika sehemu zenye mafuta kama kwenye paji la uso na pua. Usisugue sehemu inayozunguka macho yako.

Then again chukua kitambaa chako laini, weka katika maji ya uvuguvugu na usafishe uso wako vizuri hadi scrub yote iishe.

3.STEAM YOUR FACE / TUMIA MVUKE.
Baada ya exfoliate, hakikisha umeshataarisha maji ya moto kabisa ili uweze kutumia mvuke wake. Chukua na taulo au nguo yoyote nzito, jifunike nayo kichwani kisha inamia katika beseni lako lenye maji ya moto. Unaweza ukaongezea rosemary au mint au herb yoyote uipendayo katika maji hayo. Kaa kwa dakika 10 ili pores zako zifunguke.

4.APPLY A MASK / PAKA FACIAL MASK.
Baada tu ya kusteam uso wako, pore zitakuwa zimefunguka, now chukua mask upendayo kuitumia, au unaweza kusearch humu humu katika blog na ukapata different facial mask. Paka mask na ukae nayo kwa dakika 10-20, au inategemea na mask yako inasema ukae nayo kwa muda gani. Usipake katika sehemu inayozunguka macho yako.

Kwa wenye ngozi yenye mafuta, ni vizuri ukitumia mask ambayo inanyonya mafuta, kama vile clay mask, ili kuweza kupunguza mafuta usoni.

5.MOISTURIZE YOUR FACE / PAKA MAFUTA AU LOTION YA USO.
Baada ya vyote hivyo, paka moisturizer ili kulainisha uso wako. Unaweza ukawa na moisturizer yako maalum, kuna wengine wanatumia mafuta ya nazi, olive oil au hata vaseline tu kama mimi.

Then acha uso wako upumue for the rest of the day bila makeup wala makorokocho mengine.
Feel free kuacha comment, kuuliza maswali na kuongezea point ulizonazo.
FOLLOW US KWA INSTAGRAM :: BONGOUZURI
TWITTER :: BONGOUREMBO

You Might Also Like

2 comments

 1. thanks again mana mie nilikuwa n mmoja wa watumiaji wa sabuni za kawaida kwa uso ila kwa kutumia maji ya uvuguvugu.
  1.naomba unisaidie mie nina ngozi yenye mafuta usoni naweza kutumia cleanser gani?
  2.je mwenye ngozi ya mafuta kama mie atumie scrub gani?
  3.je mtu anaweza tumia facial mask yyt bila kujali aina y angozi yake?

  asante kwa msaada wako

  ReplyDelete
 2. asante my dear hata mimi nilikua mtumiaji maarufu wa sabuni usoni nikawa natoka vidoadoa na ngozi ya uso haivutii kabisa nimenunua face wash ya acnes,toner yake pamoja na tube ya kupaka ya acnes kwa ajili ya madoa sasa hvi angalau kidogo.nikimaliza hii nitaanza hizi step by step

  ReplyDelete

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.