, , ,

MATUMIZI YA APPLE CIDER VINEGAR KATIKA UREMBO WAKO.

12:59:00 PM


Apple cider vinegar imekuwa ikitumiwa kwa vitu vingi sana, na urembo pi ni moja wapo. Kuanzia kuonoa chunusi, kufanya nail polish ikae muda mrefu, ku-tone ngozi yako nk. Ingia HAPA na HAPA kusoma post zinazoelezea jinsi ya kutumia apple cider vinegar kuondoa chunusi na kufanyia facial.

MATUMIZI YA APPLE CIDER VINEGAR::
1.Skin Soother

Inasaidia ngozi yako kama unawashwa, mimina apple cider vinegar kidogo katika bathtub yako yenye maji ya uvuguvugu na ukae ndani kwenye maji kwa dakika 15. Ita-restore pH balance ya ngozi yako.

2.Face Toner.

Unaweza pia kutumia apple cider vinegar kama toner yako. Changanya kijiko 1 cha apple cider vinegar na vikombe 2 vya maji masafi ili kui-dillute ,NEVER use apple cider vinegar yenyewe kama ilivyo usoni! Tumia pamba kupaka uso ukiwa msafi, itasaidia kukaza uso ili usiwe na mikunjo.

3.Hair rinse.

Pia unaweza kutumia kwa nywele zako. Chukua vijiko 2 vya appl cider vinegar changanya na kikombe 1 cha maji. Ukisha osha nywele zako kama kawaida chukua huu mchanganyiko na ulowanishe tena nywele zako kisha fuata na conditioner kidogo, then osha lightly na maji ya kawaida. Itasaidia kuondoa uchafu uliobaki na kuzifanya nywele zako zing'ae.

4.Razor bump remedy.

Ukijichuna na kiwembe, au ukajikata ukiwa una-shave,paka kwanza asali na ukae nayo kwa muda kidogo , osha then chukua pamba na udumbukize katika apple cider vinegar ambayo haijachanganywa na maji, kisha pitisha katika hiyo sehemu uliyojichuna.

5.Dundruff treatment/Huondoa mba.

Changanya kipimo sawa cha apple cider vinegar na maji, massage katika nywele zako kabla haujaziosha. Au unaweza kuchanganya apple cider vinegar katika shampoo yako na ukatumia kuosha nywele zako kama kaawaida.

6.Foot deodorizer/Huondoa harufu mbaya ya miguu.

Changanya kikombe 1 cha apple cider vinegar na vikombe 4 vya maji katika baseni. Loweka miguu yako kwa dakika 15. Kisha nawa kwa maji ya kawaida ikaushe na ipake moisturizer. Pia unaweza fanya hivi kama una fungus miguuni.

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.