, , , , , ,

UMEPANGA KUFANYA MAKEUP YAKO MWENYEWE FOR YOUR WEDDING DAY? SOMA HIKI.

3:12:00 PM


Sio kila bride anataka makeup artist siku ya harusi yake, kuna wale wanajijulia wenyewe kupaka makeup, nobody knows your face better than you do, so sio ajabu kama unataka kujipaka mwenyewe makeup.

 Kupata a perfect complexion siku ya harusi yako, make sure unaanza kutumia skincare products ambazo ni lightweight, ina hydrate ngozi yako, ambayo haitokuwa inafanya makeup yako kuyayuka. Kuna zile skin care products ambazo zinahakikisha makeup yako inakaa for a whole day.

SPF katika sunscreen inaweza ku-affect your pictures siku ya harusi yako..lakini kama unafunga ndoa on the beach ni lazima kupaka sunscreen. Chagua sunscreen ambayo SPF yake haipo juu ya spf 15..hii iatsaidia hata picha zikipigwa na flash uso wako usitokee kama jini.

Hakikisha unablend bronzer yako vizuri in a way kwamba uso wako pamoja na shingo yako rangi zake zitamatch..na tumia foundation inayoendana na rangi yako! hutaki kuweka kumbukumbu ya kuwa na rangi mbili tofauti on your bigday jamani.

Siri ya kupata the perfect blush shade ni kutafuta rangi inyoendana na rangi asili ya lips zako. Apply bush ya kutosha na get the photographer akupige pictures wakati unafanya makeup asubuhi ili uone ni kipi unatakiwa kurekebisha..pia piga picha katika mwanga tofauti, ndani na nje, na flash na bila flash.

 Kila kitu kipo kwenye details. Tumia color corrector au concealer ili ku-brighten area inayozunguka macho yako, sanasana chini ya macho.

Kama unataka kupaka red lipstick on your wedding day, unatakiwa kufikiria kuhusu texture, shiny au creamy textured lipstick zitaishia kwenye glass yako ya champagne. Tumia kidole chako kupakia na kisha u-dust a little powder kwa juu ili ikae kwa muda.

Usipake a glossy red lipstick, glossy sio kiss proof hivyo mtaishia kupakanatu.
Kwa nyusi zako, ni bora kutumia gel au pencil kujaziliza nyusi zako. Fuatiliza shape ya nyusi zako ..soma HAPA kwa maelezo zaidi.

Always tumia eyelash curler kabla ya kupaka mascara. Paka kwanza mascara ya kawaida kwa both sides the kabla hazijakauka paka a gel-based waterproof mascara kwa juu ili ikae kwa muda mrefu.

Kama hujawahi kuvaa kope fake na unataka kuzivaa katika siku ya harusi yako, basi jaribu kuzivaa angalau week 1 kabla ya harusi yako na uone kama utapenda kuzivaa au la.


TIP :: ukilia, wengi huwa wanalia on their big days, tears of joy! Ok so,ukilia ni lazima ubebe wipes zako, wipe au dab your tears kwenda juu sio chini! or else utapata mstari usoni.


Ukiwa unapaka eye makeup, weka kioo chini ya kidevu chako ili uwe unaangalia kwa chini.

Kuna watu wanaenjoy doing their own makeup lakini kama unaona kama itakustress tu ni bora kuhire a makeup artist ambaye umeshaona kazi zake. Na huyo makeup artist pia akufanyie makeup kabla ya siku ya harusi ili ujue exactly ni vipi unataka makeup yako kuonekana siku hiyo. It is your big day na it should be beautiful and memorable.

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.