Jinsi Ya Kuondoa Alama Za Sidiria Mwilini, Alama Zinasababishwa Na Nini?

3:51:00 PM


Hello Loves, nimepokea swali ambalo huwa linawasumbua wadada wengi. Hizi alama zinazotokea kwenye mabega au mgongoni, alama za sidiria. Alama inaweza kukutokea ikwa ni rangi nyeupe kuliko rangi ya ngozi yako au ikaweka weusi.
Now, hii inatupa ugumu, unakuwa huwezi kuvaa hizi trend zetu za kisasa kama vile off-shoulder na backless styles, maana hizo alama zitakua zinaonekana.
Kabla hatujaenda kwenye njia za kuondoa alama hizo, tuangalie sababu ambazo zinafanya upate alama za sidiria.


1.Material ya bra unayoivaa inaweza isiwe suitable for your skin, yani ngozi yako na material ya bra yako havipendani. Inaweza ikakuletea irritation / muwasho ndio maana unakuta unajikuna, ukiongeza na joto basi ndio kabisa.

2.Bra isiyokutosha pia inaweza ikawa ni sababu ya kutokewa alama. Bra ikikubana inazuia mzunguko wa damu, inaharibu tissue ya ngozi sehemu hizo zilizobanwa na kufanya ngozi kutokewa alama. Alama zinazotokea kwasababu bra inakubana huwa ni ngumu sana kuondoa.

Endelea kusoma nikujuze zaidi natural remedies ambazo zitaonda alama hizi.
Kama umewahi kusikia kuwa mwili wako mzima utunze kama unavyoitunza sura yako. Kama ni scrub, mafuta, na vingine mwili pia unahitaji mafunzo hayo hayo.

NATURAL REMEDIES.
1.Vaa Bra size yako.

Sidiria inatakiwa ikutoshe vizuri, kwenye mabega na kwenye mzunguko, haitakiwi kukubana bali iwe fit! Tafuta the perfect bra size ambayo hata ukishinda nayo siku nzima unakuwa comfortable, maana kuna wengine bra zinawabana haswaa kiasi cha kwamba mtu circulation inakata kabisa na hata damu kuvilia.
Kama hujui size ya bra yako, unaweza kuuliza kwa ma-pro wanaofanyaga bra fitting, watakusaidia kutafuta bra zinazoku fit vizuri na bra for every occasion.

2.Tumia Milk Pack.

Milk pack ni mchanganyiko wa maziwa fresh na almond oil. Chukua mchanganyiko huo na upake kwenye sehemu ulizotokewa alama. Fanya ku massage pole pole kisha jifunike na taulo kwa dakika 10, kisha nawa kwa maji ya uvuguvugu. Paka moisturizer yako kama kawaida.
*Kwa matokea mazuri na ya haraka usitumie sabuni katika sehemu zenye alama.

3.Exfoliate.

Hapa ni kama unavyofanyia scrub uso wako ili kuondoa ngozi iliyokufa. Unaweza kutumia scrub yako unayotumia usoni. Lakini kwa scrub ambayo inaondoa weusi na kulinganisha rangi ya ngozi yako tumia lemon and sugar scrub / Scrub ya ndimu na sukari. Fuata step za kawaida za kufanya scrub.

4.Oil Massage.

Tumia virgin Olive oil, Almond oil, lavender oil, Tea tree oil au essential oil yoyote unayoipenda kufanyia massage sehemu zenye alama, na zitaanza kupotea pole pole.

5.Tumia Sunscreen.

Kama wewe ni mpenzi wa kuvaa kata mikono, then nadhani utakuwa ume-notice kuwa baada ya siku ndefu ya mizunguko zile sehemu ambazo umefunika zitakuwa na alama ya bra, hapa ndio ngozi yako inakua nyeupe kushinda sehemu nyingine. Tumia sunscreen ili uweze kujilinda na sunrays. Tfuta sunscreen yenye SPF 15 au zaidi.

6. Yogurt And Tumeric Pack.

Huu ni mchanganyiko wa yogurt na manjano. Changanya vizuri kisha massage sehemu zenye alama, Nawa na maji ya uvuguvugu then paka moisturizer. Endelea kutumia kila siku kwa wiki 1 kuanza kuona mabadiliko.

7. Kunywa Maji Ya Kutosha.

Au kama wewe sio mtu wa natural remedies unaweza kutumia "fade cream" ambazo zitasaidia kuondoa alama hizo, always tafuta fade cream zenye natural ingredients kama vile kojic acid, Vitamin C na licorice extract.
Itakuwa vizuri zaidi kama utapata straight kutoka kwa daktari wa ngozi, usiende tu kununua cream yoyote ukaishia kujiharibu zaidi.

Kuwa huru ku-share na sisi huwa unatumia njia gani kuondoa alama za bra kama zimewahi kukutokea, inwezekana kuwa njia yako ni nzuri zaidi au unafahamu cream nzuri za kutumia kuondoa alama hizo, and also kwa watakao tumia nyia hizi nilizowaletea leo, tuambie results.

You Might Also Like

1 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.