, ,

Health Issues : Bleeding During Ovulation / Kutokwa Damu Katikati Ya Mwezi.

11:13:00 AM


Hi Ladies, leo let's talk about something ambacho najua wanawake wengi sana kinawatokea. Kutokwa damu kipindi cha ovulation. Unless umeshaenda kwa daktari na kuelezewa ni kwanini hali hii hutokea nadhani utakuwa hujui. Basi tujuzane kuhusu hiko,

Ovulation ni kile kipindi ambapo yai linaachiwa kutoka kwenye ovary na kupita kwenye fallopian tube, hapa ndio vitu viwili vyaweza kutokea, either utapata mimba if you have sex katika siku hizi au siku zikipita hujapata mimba bas baada ya siku kadhaa utapata period yako.

Siku za ovulation zinatofautiana kwa kila mtu, mwezi mwingine zinawahi, mwingine zinachelewa. Unaweza kujua kama una ovulate kwa kufanya test au kwa wanawake wengi huwa wanatokwa na damu (spotting) kidogo, inakua sio kama ile ya period na unaweza pia ukasikia maumivu. Lakini wanawake wengine huwa hawahisi chochote.

Inasemekana kuwa kwa wanawake wengi kipindi cha ovulation huwa ni Kati Ya siku ya 11 na 21 ya mzunguko. Kama unajua kuhesabu siku zako basi itakua rahisi kujua na hata kujipaga unapotaka kupata mtoto.

Dalili za ovulation.
1. Maumivu upande wa kushoto kwa wengi.
2. Kutokwa kwa damu kidogo siku 3-5. Inakua rangi ya pink, red au brownish. Haiwi nzito kama ya period.
3. Wengine husikia kichefuchefu.
4. Kutokwa na cervical mucus.

Kutokwa kwa damu kipindi cha ovulation ni kawaida kabisa na inasemekana kuwa ni afya, hata kama haitokei kwa wanawake wore. Lakini ikiona kwamba damu inazidi kutoka hata baada ya ovulation ni vizuri kuenda kumuona daktari. Baada ya ovulation unatakiwa kukaa siku kadhaa kabla hujapata period.

Haya ni maelezo kwa ufupi tu.
**Lakini pia Kutokwa na damu  (spotting) ni moja ya dalili ya early pregnancy.**

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.