, , ,

Jinsi Ya Kutengeneza Oatmeal Facial Mask.

1:55:00 PM


Last Sunday nilisema I am trying out a new #DIY Facial mask, ni rahisis sana kutengeneza na it turns out kuwa ni nzuri sana. Oatmeal inasaidia ku rejuvinate ngozi yako na although it has only been a week nimeona mabadiliko kwa mbali.
Kwasababu I have oily skin nilianza kwa kunawa uso kawaida tu na maji ya uvuguvugu ili kuondoa uchafu.

Then nikatumia a simple #DIY scrub ambayo ni kipande cha ndimu na sukari. Nimesugua polepole kwa kama dakika 5 kisha nikanawa kwa maji ya uvuguvugu. Nikakausha uso kwa kutumia taulo laini, hili ni la uso tu.
Then nikapaka mask yangu niliyokwisha iandaa.


Jinsi Ya Kutengeneza.
Chukua Oatmeal, nimetumia Quaker oatmeal unaweza kupata supermarket. Weka maji ya moto kisha anza kukoroga hadi iwe nzito kabisa. Kamulia ndimu nusu endelea kuchanganya then acha ipoe. Ikishapoa chukua kijiko kimoja kidogo cha mdalasini then changanya vizuri, kama imekua nzito sana ongeza maji kidogo.
Paka mchanganyiko huo uso mzima na hata kwenye shingo, usipake sehemu iliyozunguka macho. Kaa nayo kwa dakika 20-30. Nawa kwa maji ya uvuguvugu, jikaushe vizuri then paka moisturizer kisha acha ngozi yako ipumue for the rest of the day.

Unaweza kufanya hivi mara 2-3 kwa wiki.

Kumbuka kama una ngozi yenye mafuta kuwa muangalifu na moisturizer unayotumia. Tafuta moisturizer ambayo inaiacha ngozi laini lakini sio kuteleza.

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.