Njia Za Kusafisha Pores.

1:53:00 PM


Hello Loves, kwa anayejua pores kwa kiswahili Ni nini tuambizane. Anyways leo tuangalie Njia ambazo unaweza Kusafisha pores usoni ili kuweza kuepusha vipele na chunusi na kuwa na uso laini na msafi.
Pores zako zikiwa zimejaa uchafu ndio ngozi yako inaonekana kama ina matobo matobo, kama hivi


Tumia Kati Ya Njia Zifuatazo:


1. Tumia baking soda, chukua vijiko 2 vya baking soda changanya na kijiko 1 cha maji, paka usoni na ufanye kumassage pole pole kama unavyofanya scrub. Acha kwa dakika 5 kisha nawa kwa maji ya uvuguvugu. Fanya hivi mara 1 kwa wiki. Itasafisha uso, kuondoa uchafu na kulinganisha rangi ya ngozi yako.

2. Tumia ndimu, chukua kipande nusu cha ndimu paka usoni kwenye sehemu unazoona zipo affected. Acha ikae dakika 5 kisha nawa. Fanya hivi mara 1 kwa wiki.

3. Tumia cleansing brush. Hizi cleansing brush zinasafisha vizuri sana. Zinawasaidia hata wale wenye chunusi kuondoa uchafu na kufanya uso use safi kabsa.

4. Tumia Black charcoal mask. Hizi mask zinaondoa black heads na white heads na kuacha pores safi.

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.